Wednesday, June 13, 2018

Anaandika ndugu Nangolingo kapolo kuhusu urithi wa teknolojia kwa vijana wa generation web2.0 
 Nitangulize samahani kwanza. Nina POVU nataka nilitoe. Gazeti ni refu kidogo.
Naanza kama ifuatavyo:
Sisi vijana tuliozaliwa miaka ya 80, tunao wajibu mkubwa sana wa kukaa chini na wadogo zetu ambao kwa bahati mbaya ama nzuri wamezaliwa kipindi cha utandawazi. Kipindi ambacho hata mwanafunzi wa shule ya msingi anao uwezo wa kumiliki simu.
Kukua katika kipindi cha utandawazi inaweza kuwa bahati mbaya ama nzuri, sababu upatikanaji wa taarifa ni rahisi sana - yaani taarifa zote - zinazoweza kujenga ama kubomoa.
Hakukuwahi kuwa na wakati mwingine ambapo upatikanaji wa elimu na ujuzi uliwahi kuwa rahisi kama ilivyo sasa. Wadogo zetu wana bahati ya pekee kukua katika nyakati ambazo unaweza kujifunza chochote kile unachotaka, kwa bei rahisi sana ama bure kabisa.
Nawaonea wivu sana. Wakati mwingine natamani kama ingewezekana kubadilishana nafasi. Na mimi niwe teenager kipindi hiki, niweze kujifunza vitu vingi angali nikiwa bado mdogo.
Maana wakati kipindi mimi niko teenager, nilibahatika tu kuwa na "keyboard" ya computer. Lakini niliweza kujifunza ku type kwa kutumia vidole vyangu vyote kumi, pasipo kuangalia keyboard. Nawaza tu, kama kipindi kile ningekua na laptop kama wadogo zangu leo, sijui ningefika wapi.
Kipindi kile nina "volunteer" kusimamia internet cafe ili jioni waniruhusu kutumia internet masaa mawili ili niweze kujifunza kidogo programing, huku natumia kitabu cha AmigaBasic cha mwaka 1986. Kitabu cha AmigaBasic cha mwaka 1986 na teknolojia ya 2001, wapi na wapi! Ni shida tupu!
Nilitumia mwaka mzima kujifunza kitu ambacho leo pengine ingenichukua wiki tu. Mazingira hayakuwa rafiki kabisa. Upatikanaji wa maarifa ulikua duni sana.
Nilipomaliza Form Six, nilipata 'party time' wakati wa 'Likizo ya Mkapa' - kwenye ofisi ambayo kulikua na computer na internet. Hiyo ndio ikawa fursa yangu ya kujifunza, nikatenga muda kuanzia saa 11 jioni, baada ya kazi, hadi saa 3 usiku, ndio narudi nyumbani.

Miezi minne baadae, nikaandika programu yangu ya kwanza. Hiyo ndio ikaniingiza kwenye consultancy business hadi leo. Ndio ilikua inanipa boom chuo na kuacha matumizi nyumbani.
Miaka 15 baadae, mazingira yamebadilika sana. Internet ipo kila mahali, spidi kubwa, bei rahisi ya kutupa.
Juzi nimeona Kingstone wametoa FlashDisk ya 1Terra Byte, nikakumbuka zile Floppy Disk zangu za 1.44MB nilizokua nimejaza chumbani, nikatamani kulia. Siamini wadogo zetu wanakua katika mazingira ya anasa namna hii.
Lakini nasikitika sana kuona wadogo zangu wanatembea mtaani na hard disk za 5 Terra Bytes, zimejaa movies, series pamoja na Video Games. Hakuna hata kitabu kimoja?
Hivi mtu ana Terra Bytes mbili zimejaa series! Anaziangalia saa ngapi? Wadogo zetu wamekua kama 'Netflix' inayotembea.
Miaka 15 baadae, bado wadogo zetu wanatoka chuo kikuu, hawajui hata kuandika CV. Computer Science graduate hawezi kutengeneza hata program ya calculator!?
Wanafunzi wanafeli sababu hakuna waalimu na huku mikononi wameshika smartphones zimejazwa bando la kuingia Insta!?
Online video courses zipo kila kona, hulipii chochote zaidi ya bando lako la 500. Lakini bado, hata kujifunza kiingereza kidogo ni shida? Wanaishia kuingia tu Instagram hadi unamaliza chuo, huwezi hata kufanya interview kwa kiingereza?
Kuna haja ya kuwamwagia maji baridi wadogo zetu, waamke kwenye usingizi wao wa pono.
Kama si sisi kaka zao na dada zao wa kuwakumbusha kuwa wanaishi katika nyakati za dhahabu na almasi, nani mwingine wa kuwakumbusha?
Tuwakumbushe kuwa, kuna takribani watumiaji 1.9 milioni Instagram, na zaidi ya 6 milioni Facebook toka Tanzania peke yake. Hiyo sio tu fursa ya kuchati na marafiki wapya, bali hiyo ni fursa pia ya kufanya biashara.
Fikiria leo umepewa nafasi ya kuposti sehem yenye wasomaji milioni sita. Ungeposti kitu gani?
Lakini hata hivyo, bado vijana wetu wanasema hakuna fursa za ajira.
Umeshaambiwa kuwa watanzania 1.9 milioni wanatumia instagram, bado fursa ya kupata hela ya kujinunulia shati huoni?
Babu zetu waliishia kujenga nyumba za udongo. Wengi hawakuwahi kumiliki gari, achilia mbali kupewa lifti.
Wakaja baba zetu, ambao walizaliwa miaka ya 1940 na 50, wengi walimiliki magari wakiwa na umri wa mika 40, wakajenga nyumba wakiwa na miaka 50, wengine hadi miaka 60 ndio wakamaliza kuweka madirisha.
Sisi watoto zao, tukaweza kuendesha magari yetu tukiwa na miaka 20 huko, tukajenga tukiwa na miaka 30.
Sasa, nyie wadogo zetu ni zaidi hapo. Kwa fursa zilizopo, mnatakiwa kwenye mid 20's muwe mmeshajenga na kuhamia makwenu.
Mkimiliki nyumba mkiwa na miaka 30 huko kama sisi, tutawacheka sana. Sababu mmelala usingizi wa pono, mmeweka mbele mambo yasio na maana wala faida kwenu.


No comments:

Post a Comment

 *AGRIBUSINESS & AGRICULTURE*  When most people think of agriculture in Africa, images of poor and overworked farmers with crude to...