Wengi tumelipa tafsiri tofauti neno hili bila kutafiti na kudadisi kwa kina nini maana yake. Katika kufahamu hilo yatupasa kila mmoja wetu kujua lengo la uumbwaji wake katika dunia hii, tunasadiki ya kwamba muumba wetu ni mmoja aliyetukuka na haikua kama tulivyoelekea sisi kutenganishwa kwa dini, kabila au namna yoyote itakayojenga tofauti.
Hebu fikiria unadiriki kukatisha maisha ya mtu hali ya kua wewe mwenyewe unatamani kuishi, ifahamike kua 'kila nafsi inaitamani kesho hali kwamba kesho haifahamiki' maana kwamba hakuna anayependa maisha yake yakatike bila hiari yake. Usipende kumfanyia mtu jambo usilopenda kufanyiwa, vipi unakejeli mtazamo huo na kufanya ovu?.
Tujitambue binadamu kama ambavyo baba husikia fahari kwa mwanae akifanya jambo jema basi na hata MUNGU atamsitiri na kumsalimisha yule mwenye kufanya yanayompendeza.
Maneno kama "wakubwa wakiamua jambo kua linakua, kuchukua mali kwa tajiri kwenda kwa masikini (mfumo gani huo?!,) mfumo wa kishetani." alisema Mwl J K Nyerere R.I.P tunayadharau na kua na kauli zetu za kishetani kusema "pesa inaongoza dunia (money Run the World)" ni hivyo tulivyoagizwa na MUNGU tuyafanye duniani?
Jiulize nani anaemjaalia binadamu pumzi, jua, chakula, maji na neema nyingine zisizoisha daima ashindwe kumjaalia mazuri binadamu anayoyatamani, hatukuagizwa kuishi hivi tutaangamia tukikejeli haya.
MAISHA ni kufahamu nani aliyekuumba na kwanini uliumbwa, kufanya yaliyo mema na kukatazana mabaya, kutoitambua chuki katika maisha yako, kuthamini na kujali viumbe wote duniani bila kuangalia mapungufu yao (utaulizwa kwanini ulikatisha maisha ya sisimizi/
KUFA ukiwa unaokoa maisha ya kiumbe mwenzako mfano (kumuokoa mfa maji ufe wewe, inaonekanaje hiyo?) sio kufa kwa kujitoa mhanga na kupoteza roho za wengine wasio na hatia, usimuache mwenzako ahatarishe maisha ili ujiokoe wewe kwani hata siku ya mwisho MUNGU hatokuokoa.
Penda kila kilichoumbwa na MUNGU sio kilichoundwa na binadamu, mpende kila unaemuona ili tuishi kwa amani ufike wakati tulale milango wazi bila kujali kwani MUNGU yupo pamoja nasi.
Jina lako ni BINADAMU> bin ADAMU wote ni wana wa Adam, usiseme mimi mkristo,muislam
NA HIYO NDIO SIRI YA MAFANIKIO YETU AFRIKA NA DUNIA NZIMA.
Tuwe pamoja, MUNGU IBARIKI TANZANIA, IBARIKI AFRIKA, IBARIKI NA DUNIA NZIMA. Nawapenda wote
No comments:
Post a Comment