1: MYUS.COM link- MyUS.com –
International Shipping, Mail and Package Forwarding Service – MyUS.com hii ni kampuni niliyoitumia na nina uzoefu nayo ya mizigo miwili, hawa ni waaminifu wanatoza pesa kidogo na huwa hawachukui muda kukutumia mzigo wako. Yaani unafika leo hata ukitaka utumwe leo unatumwa, na utafika kwa upesi sana bila ya zengwe lolote.
Ubaya wao: wanatumia sana DHL ambayo kwa mizigo mikubwa ni gharama sana kwa mtanzania wa kawaida, kiasi cha dola kumi kujiunga kama sikosei na huduma zao Uzuri wao: watakutumia mzigo hata kama utakuwa hauna pesa kwenye account yako, watakujulisha ni duka lipi lina discount ya kutumia huduma zao, watakukumbusha kulipa deni lao, utapewa muda wa miezi miwili kulipa pesa yao,
2: COMGATEWAY
comgateway.com/ hawa pia ni forwarding company nzuri sana, nimepitia site yao na kuona wana policy nzuri sana,cha kwanza ni sales tax- free U.S. online shopping yaani punguzo la kodi ya kufanya manunuzi Marekani,hii inapelekea huduma zao kuwa nafuu zaidi,pia wana ushirika na shipping courier DHL na FEDEX hivyo kufanya huduma zao kuwa rahisi zaidi. Pia wanakupa habari kuhusu discount za masoko mbalimbali kama myus.
3: BORDERLINX
Link- Buy in the USA, ship to Belgium with Borderlinx hawa pia ni wazuri sana na hawana tofauti sana na stackry ,wanawiana ingawa ni competitors wakubwa hivyo inakupa urahisi wa kuwatumia,hawa pia hawana registration fee na wanakupa uchaguzi tofauti tofauti za kutumiwa mzigo wako.
4: SHIPITO
Link- USA Address & Mail Forwarding – Shipito.com hii pia ni kampuni kongwe ya forwarding na wao gharama zao ni nafuu sana ingawa wanapokea malalamiko mengi sana kutoka kwa wateja wao ukiangalia kwenye forums nyingi.
Ila kiujumla ni wazuri kwasababu malalamiko ni madogo kulinganisha na ufanisi na pia wanajua na ni wazoefu sana na kazi yao
5: STACKRY
Link- Stackry – US shopping, global shipping hii nayo haina tofauti na myus isipokuwa hawa wao hawana kiasi cha kulipia kujiunga nao na wao pia wanakupa option nyingi za kutumia mizigo yako na mambo yao pia ni mazuri kulinganisha na comment wanazopokea kutoka kwa wateja wao.
Jamani ni hayo tu niliyo nayo, kazi kwenu ni kufanya utafiti na pia kuangalia na kuchunguza mambo kabla ya kuchukua uamuzi.
Sehemu ya tatu na ya mwisho kuhusu namna ya kufanya ununuzi kupitia mtandaoni.
No comments:
Post a Comment