Friday, June 8, 2018

Je ipi ni Njia Nzuri Ya Kununua Vitu mtandaoni kwa maana ya (Online ) kama vile Ebay,Amazon , Ali Baba Na Best Buy.
Kumbuka tu imekuwa ni shida sana kwa sisi hasa watanzania tulio wengi kununua bidhaaa katika masoko haya ya mtandaoni kwani mengi huwa hayakupi fursa ya kutumiwa mzigo wako moja kwa moja Tanzania.
Nimejaribu kupitia pitia forums nyingi nichanganue namna mbadala ya kupata mizigo bila ya kutumia gharama nyingi.
Hii ni kwa kutumia FORWARDING COMPANIES ambazo kazi yake ni
a) Kukupatia anuani ya Marekani (au popote iliopo ila nashauri Marekani au Uingereza) au US Shipping Address
b) Kupokea mzigo kwenye soko ulilotumia ( Amazon, EBay au lolote lile lisiloship Tanzania)
c) Kukutumia mzigo wewe hapo ulipo kwa wakala kama DHL, FEDEX, UPS, USPS nakadhalika baada ya kujua kazi ya forwarding company unahitaji kuwa na vigezo vifuatavyo .
1: CREDIT CARD (KADI YA BENKI) INAYOFANYA ONLINE PURCHASES;
Hii inapatikana karibu benki zote hapa Tanzania ni kadi yeyote ya visa au MasterCard unachotakiwa ni kwenda kwenye tawi la benki yako na kuomba fomu ya kuruhusu kadi yako ifanye malipo ya mtandaoni (online purchases) na mara nyingi huchukua maximum masaa 24 ku activate.
2: KUJIUNGA NA PAYPAL
Hiii ni kampuni inayolinda malipo yako kwa kutomuonesha muuzaji details (nyaraka) za kadi yako kama number na css ambayo vitampa muuzaji access ya kuchukua pesa zako. Ila kwa PayPal utalindwa na kurudishiwa pesa pale panapotokea shida au huduma mbaya.
3: KUJIUNGA NA FORWARDING COMPANY
Hii hatua ni ya wewe kwenda kwenye website (tovuti) za hizi forwarding company na kujiunga(signup) nazo/nayo ili zianze kukupatia huduma.Nitaelezea chini zaidi kuhusu ipi ni ipi na huduma zao zikoje na faida na hasara za kila moja ili ujichagulie wewe mwenyewe binafsi .

Wakati ujao nitaziorodhesha kampuni zenyewe na taarifa zao

No comments:

Post a Comment

 *AGRIBUSINESS & AGRICULTURE*  When most people think of agriculture in Africa, images of poor and overworked farmers with crude to...